
>>> JESHI LAENDELEA KUMSAKA
JESHI
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi
hilo aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless
Lema ametoroka.
Msemaji
wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua
yake ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ili
kumhoji na kujiridhisha kama kweli ni mwanajeshi wake kabla ya
kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kifungu cha 147 cha Katiba
ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977.
“Huyu
kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),
lakini wakati tunaendelea...