Unordered List

Pages

Friday, September 28, 2012

CCM YASHINDA UMEYA JIJI LA MWANZA

UFAFANUZI KILICHOTOKEA KWENYE UCHAGUZI WA UMEYA WA JIJI LA MWANZA KATI YA CCM NA CHADEMA.

Mgombea wa kiti cha umeya katika Halmashauri ya jiji la Mwanza kupitia CCM na diwani wa kata ya Mkolani Ndg Stanslaus Mabula, ameshinda kiti cha Umeya wa Halmashauri ya Nyamagana kwa jumla ya kura 11 dhidi ya mgombea wa CHADEMA diwani wa kata ya Mahina Ndg Charles Chibara aliyepata kura 8.

CCM wameshindishwa na mbinu za kisiasa amabzo uhalali wake kisheria linabaki kuwa suala la wanasheria wanaojua taratibu zikoje kutufafanulia.

Baada ya mgawanyo wa Halmashauri ya jiji la Mwanza na kuwa na halmashauri ya jiji inayoundwa na Majimbo mawili, kulipatikana Halmashauri ya Nyamagana inayoundwa na Jimbo la Nyamagana na halmashauri ya ilemela inayondwa na jimbo la Ilemela.

Mgawanyo huo ulifanyika Mwezi Julai mwaka huu ambapo Mgawanyo wa Madiwani ukabaki ifuatavyo;

NYAMAGANA.

CHADEMA - MADIWANI WA KUCHAGULIWA - 5, MADIWANI WA VITI MAALUM - 2, MBUNGE - 1. JUMLA CHADEMA WANAKUWA NA WAJUMBE 8 WA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA NYAMAGANA.

CCM - MADIWANI WA KUCHAGULIWA - 6, MADIWANI WA VITI MAALUM - 1, MBUNGE - 0. JUMLA CCM WANAKUWA NA WAJUMBE 7 WA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA NYAMAGANA.

CUF - DIWANI WA KUCHAGULIWA -1, DIWANI VITI MAALUM -1, MBUNGE 0. JUMLA WANAKUWA NA WAJUMBE WAWILI WA BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA NYAMAGANA.

ILEMELA.

CHADEMA - MADIWANI WA KUCHAGULIWA - 6, MADIWANI WA VITI MAALUM - 2, MBUNGE - 1. JUMLA CHADEMA WANAKUWA NA WAJUMBE 9 WA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA ILEMELA.

CCM - MADIWANI WA KUCHAGULIWA - 3, MADIWANI WA VITI MAALUM - 2, MBUNGE - 1. JUMLA CCM WANAKUWA NA WAJUMBE 6 WA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA ILEMELA.

CUF - DIWANI WA KUCHAGULIWA - 0, DIWANI VITI MAALUM - 0, MBUNGE 1. JUMLA WANAKUWA NA WAJUMBE WAWILI WA BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA ILEMELA.

Thursday, September 27, 2012

ZITTO KABWE KUGOMBEA URAISI 2015

Mbune wa Kigoma  mh. ZITTO KABWE athibitisha kwamba atagombea URAIS 2015,   hayo ameyasema wakati akihojiwa na mwendesha kipindi cha amplifire Millard Ayo. Zitto kupitia amplifer ya CLOUDS FM akasema ya kwamba Atagombea kupitia CHADEMA kwa hivyo wale mlio na wasiwasi huo ndio ukweli.
Asema kuna watu wanajidai wao ni CHADEMA zaidi ya wengine wakati yeye amekuwa mwanachama wa CHADEMA tokea ana miaka 16......
Miaka 10 ya ubunge inamtosha hivyo anataka kwenda hatua nyingine kisiasa na anazo AGENDA za msingi za kusimamia hivyo yeye ni tofauti na wanasiasa wengine wanaoutaka urais kama sifa 
 
source; CLOUDS FM ANPLIFER NA MILLAD AYO

COMRADE SAMABALA AGOMBEA UENYEKITI WA UVCCM MKOA WA DODOMA

       Mwanasiasa na mwanzilishi wa group maarufu la Tanuru la Fikra katika mtandao maarufu wa facebook, hatimaye amefunguka na sera ambazo zitamwingiza kwenye cheo hicho chipya endapo kama wanachama wa Dodoma (UV-CCM) watamchagua katika kinyang'anyiro hicho. na haya ndio maneno yake kwenye ukurasa wa facebook
‎>----SAFARI NDEFU YA MAFANIKIO INAENDELEA-------->

*...SHUKRANI ZANGU KWA WOTE NINAOWAPENDA...*

Ndugu zangu wana TANURU LA FIKRA Na Watanzania wenzangu wote kwa Ujumla.

Jioni ya Leo napenda kuchukua fursa hii kusema Machache kwenu.:-

1. Kwanza Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniumba mimi na akaumba na vyote vilivyomo na mwenye Kumiliki kila kitu. Mfalme wa Wafalme.

2. Pili Napenda kuwashukuru zaidi Wazazi wangu wawili kwa Kunileta duniani, kunilea kimaadili KIIMANI na Kimazingira. Hayo yote ndio yamenifikisha hapa nilipo na kufahamiana na kila Mmoja.

3. Tatu napenda kuwashukuru zaidi walimu wangu toka ngazi ya awali mpaka Chuo kikuu kwa kunifundisha na kunilea kutaaluma.

4. Na nne napenda kuishukuru Kamati Kuu ya CCM (CC) na NEC Kwa busara walizotumia na hatmaye kuniteua kuwa Mgombea wa Mwenyekiti wa VIJANA DODOMA, Na NEC kupitia wilaya ya Chemba.

Kwa kweli wamenipa Heshima kubwa sana kama Kijana na Mtoto wa Masikini wa Kijijini nisiye wa Ukoo wa 'KIFALME' sitokani na Tabaka la Viongozi. Naahidi Kufanya Makubwa...

Nami Kama Sambala mtoto wa Mzee Unda wa Kijiji cha Mondo Naahidi kuilinda heshima hiyo kwa Kufanya Kampeni Kistarabu, na pia ntakapopata Ushindi basi Ntawatumikia walionipa Nafasi.

Mwisho Niwaombe wote muendelee Kuniombea na Kuniunga mkono kwa Hali na Mali ili kufanikisha ushindi wangu.

NAWAAHIDI VIJANA WENZANGU WA KITANZANIA NA DODOMA NA KONDOA/CHEMBA KUWA SITAAWANGUSHA.

NA PIA NAWAAHIDI NTAKITUMIKIA CHAMA NA UMMA NA SITAMTUMIKIA MTU KWA MATAKWA YAKE.

KWA PAMOJA TUTASHINDA..

''...ONE VOICE MANY VOTES FOR SAMBALA....''

VIJANA NGUVU YA CHAMA..

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Blogger