>>> JESHI LAENDELEA KUMSAKA
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi hilo aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ametoroka.
Msemaji
wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua
yake ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ili
kumhoji na kujiridhisha kama kweli ni mwanajeshi wake kabla ya
kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kifungu cha 147 cha Katiba
ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977.
“Huyu
kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),
lakini wakati tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba
aliyokuwa amepanga bila ya taarifa kwa baba mwenye nyumba,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:
“Askari
huyo alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga mita chache karibu na
Kituo cha Polisi cha Simanjiro, Arusha na alikuwa akijishirikisha na
ulinzi shirikishi.”
Alipoulizwa jina la askari huyo, Kanali Mgawe alijibu: “Yeye alikuwa anafahamika mtaani hapo kwa jina la kamanda.”
Hata
hivyo, Kanali Mgawe alisema jeshi hilo litahakikisha linatoa ripoti
kamili kwa umma baada ya kumkamata na uchunguzi kukamilika ili kuondoa
utata uliogubika suala hilo.
Alipoulizwa kama kuna tofauti gani kati ya mwanajeshi kuingia kwenye mikutano ya wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kisiasa kama wakuu wa wilaya na mikoa, Kanali Mgawe alijibu:” Wanajeshi wanaofanya kazi za U-DC au RC, wanaruhusiwa kisheria.”
Alipoulizwa kama kuna tofauti gani kati ya mwanajeshi kuingia kwenye mikutano ya wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kisiasa kama wakuu wa wilaya na mikoa, Kanali Mgawe alijibu:” Wanajeshi wanaofanya kazi za U-DC au RC, wanaruhusiwa kisheria.”
Alifafanua
kuwa iwapo mwanajeshi atateuliwa kufanya kazi katika taasisi yeyote ya
Serikali nje ya jeshi, atatakiwa kuvua magwanda ya jeshi na kufanya
kazi hiyo mpaka atakapomaliza muda wake na baada ya hapo ataruhusiwa
kurejea jeshini.
“Kuna
kitu kinaitwa ‘secondment.’ Mwanajeshi anaruhusiwa kufanya shughuli
zozote nje ya jeshi iwapo atahitajika kufanya hivyo. Ila kwa masharti
ya kuvua magwanda, hivyo wananchi wasishangae kuwaona baadhi ya askari
wetu ni wakuu wa wilaya na mikoa na baadaye kurudi jeshini kuendelea
na majukumu yao,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:
“Askari
akiwa katika majukumu yake mapya, atafanya kazi zote atakazopewa
zikiwamo za kisiasa kama ilivyo kwa wakuu wa wilaya na mikoa, lakini
akirudi jeshini, anarudi kuwa askari mwenye utii na kufuata kanuni za
jeshi zisizofungamana na siasa.”
0 comments:
Post a Comment