Wabunge
wa Mkoa wa Kigoma wamemtunishia misuli Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Mstaafu
Issa Machibya, kutokana na kuwatishia kuwafunga pingu kama raia wengine
wa kawaida, wakisema kauli hiyo ni dharau kubwa kwao wakiwa ni moja ya
mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la kuishauri na kuisimamia
serikali, hivyo anapaswa kuwaomba radhi.
Kanali Machibya anadaiwa kutoa kauli hiyo
mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika
kongamano la uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika, mkoani Katavi, kwa
kutamka kwamba, mbunge yeyote atakayekaidi maelekezo yake au maelekezo
ya mkuu wa wilaya atakamatwa na kupigwa pingu kama raia wengine wa
kawaida.
Wakuu wa mikoa mitatu inayounda ukanda
huo, ambayo ni Kigoma, Katavi na Rukwa, walihudhuria kongamano hilo
pamoja na wakuu wa wilaya na watendaji wengine, wakiwamo makatibu tawala
wa mikoa (RAS)na wilaya (DAS).
MOSES MACHALI
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, alisema jana kuwa kwa kauli hiyo, Kanali Machibya ameonyesha kuwadharau wabunge kwamba, ni watu wasiofikiria.
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, alisema jana kuwa kwa kauli hiyo, Kanali Machibya ameonyesha kuwadharau wabunge kwamba, ni watu wasiofikiria.
“Kwa hiyo, tunamtaka ombe radhi. Aelewe
kwamba, tunafanya kazi zetu kwa mujibu wa sheria. Hivyo, anapaswa
aheshimu mhimili wa wabunge,” alisema Machali.
Alisema kauli hiyo ya Machibya ni ya
kipuuzi na pia ni ya kifedhuli uliopindukia kwani imeonyesha mkuu huyo
wa mkoa ana uwezo mdogo wa kufikiri kinyume cha ulimwengu wa sasa
ulivyo.
Machali alisema Machibya anasahau kuwa
yeye si bosi wa wabunge na kwa hiyo, hawezi kumfunga mbunge yeyote pingu
kama anavyotamba.
Alisema kama itatokea mbunge akampinga mkuu wa mkoa, basi atakuwa ana sababu za msingi za kufanya hivyo.
Pia, alisema elimu ambayo ameipata itakuwa
haijamsaidia kitu kama hatapingana na ufisadi kama ule uliopo kwenye
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma na haitakuwa haki kama
mkuu wa mkoa atathubutu kumfunga pingu kwa sababu tu ya kupingana na
maovu hayo.
“Ibara ya 63 ya Katiba ya nchi inaeleza
kuwa kazi ya wabunge ni kuishauri na kuisimamia serikali. Kwa maana
hiyo, sisi ndiyo wasimamizi wake (mkuu wa mkoa), lazima afahamu hivyo.
Sasa huu ujasiri wa kutamka aliyoyatamka sijui anautoa wapi?” alihoji
Machali.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa Kanali
Machibya hana ubavu wa kuwafunga wabunge pingu na kusema kama atathubutu
kufanya hivyo, basi yeye na polisi watakuwa ni wapuuzi na mafisadi.
“Kwanza kuna watu wengine huwa hatutishwi.
Bungeni tunampinga waziri, na waziri hawezi kuagiza nifungwe pingu.
Sasa kwa kauli yake hiyo, nampinga Machibya. Aje kunikamata,” alisema
Machali.
FELIX MKOSAMALI
Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali, alisema kauli hiyo ya Kanali Machibya inaonyesha kuwa ana mawazo ya zamani na ya kikoloni kwani anajua fika kuwa yeye ndiye anayepaswa kufuata maelekezo ya wabunge na si wabunge kufuata maelekezo yake.
Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali, alisema kauli hiyo ya Kanali Machibya inaonyesha kuwa ana mawazo ya zamani na ya kikoloni kwani anajua fika kuwa yeye ndiye anayepaswa kufuata maelekezo ya wabunge na si wabunge kufuata maelekezo yake.
“Hawezi kuja hapa Kibondo akanielekeza mimi, anielekeza nini? Yeye ndiye aliyenichagua?” alihoji Mkosamali na kuongeza:
“Mkuu wa Mkoa amekosea sana. Mimi
naelekezwa na wananchi na sisi wabunge ndiyo tunaomsimamia yeye.
Tunakagua hadi Ofisi ya Rais. Hivyo, (Machibya) hana mamlaka hayo. Hizo
ni ndoto.”
PETER SERUKAMBA
Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, alisema Kanali Machibya amejisikia kutoa kauli hiyo kwani hadhani kama anaweza kuitekeleza kwa vitendo.
Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, alisema Kanali Machibya amejisikia kutoa kauli hiyo kwani hadhani kama anaweza kuitekeleza kwa vitendo.
“Alikuwa anafurahisha genge tu. Aliwahi
kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Mara na sasa Kigoma, je, aliwahi kumfunga
pingu nani? Kama huo ni mpango wake mpya, basi tunamtakia kila kheri
katika huo mpango wake mpya,” alisema Serukamba.
ZITTO KABWE
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alisema haamini kama Kanali Machibya anaweza kutoa kauli hiyo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alisema haamini kama Kanali Machibya anaweza kutoa kauli hiyo.
“Nachelea kutoa kauli mpaka nitakapowasiliana naye (Kanali Machibya) kujua ana maana gani,” alisema Zitto.
Alisema anasita kuto kauli kwa sasa kwa
kuwa wabunge wa Mkoa wa Kigoma pamoja na Kanali Machibya wamekuwa
wakishirikiana na kufanya kazi vizuri na kusema: “Inawezekana aliteleza
au ametafsiriwa vibaya.”
DAVID KAFULILA
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi),
David Kafulila, alisema kwa mujibu wa sheria, kinga na madaraka ya
Bunge, hairuhusiwi kumkamata mbunge katika utekelezaji wa majukumu yake
ya kibunge bila ridhaa ya Spika wa Bunge.
“Hivyo, kauli ya Kanali Machibya inaonesha
kuchoka kwake. Haya ndiyo madhara ya kuteua wastaafu kuwa wakuu wa
mikoa na wilaya,” alisema Kafulila.
Kanali Machibya anadaiwa kutoa kauli hiyo
baada ya Waziri Mkuu kusisitiza katika kongamano hilo uhusiano mzuri
baina ya wakuu wa mikoa, wilaya na wabunge.
Kanali Machibya alitoa kauli hiyo, baada
ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venace Mwamoto, kulalamika kuhusu mivutano
aliyonayo baina yake na Mkosamali.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment