Unordered List

Pages

Saturday, December 29, 2012

MNYIKA-TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nakusudia kutumia kifungu cha 10 cha Sheria ya ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kutaka nakala ya mkataba wa mkopo wa masharti kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.225 (shilingi trilioni 1.86) kutoka China. Nitataka pia nakala za mikataba wa mradi wa miundombinu ya gesi asilia ambayo itahusisha ujenzi wa mitambo ya kusafishia gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara na ujenzi wa bomba kuu la kusafirishia gesi asilia la inchi 36 kutoka Mtwara kupitia Lindi, Pwani hadi Dar es Salaam lenye umbali wa kilometa 532. Hii ni kwa sababu mpaka sasa Wizara ya Nishati na Madini haijatekeleza pendekezo nililowasilisha bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwamba kutokana na unyeti wa mradi huo kwa mustakabali wa nchi na maisha ya wananchi wa sasa na baadaye Serikali ilipaswa kuwasilisha bungeni...

Wednesday, November 28, 2012

Wabunge wa Kigoma wamtunishia misuli RC

Wabunge wa Mkoa wa Kigoma wamemtunishia misuli Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Mstaafu Issa Machibya, kutokana na kuwatishia kuwafunga pingu kama raia wengine wa kawaida, wakisema kauli hiyo ni dharau kubwa kwao wakiwa ni moja ya mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la kuishauri na kuisimamia serikali, hivyo anapaswa kuwaomba radhi. Kanali Machibya anadaiwa kutoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika kongamano la uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika, mkoani Katavi, kwa kutamka kwamba, mbunge yeyote atakayekaidi maelekezo yake au maelekezo ya mkuu wa wilaya atakamatwa na kupigwa pingu kama raia wengine wa kawaida. Wakuu wa mikoa mitatu inayounda ukanda huo, ambayo ni Kigoma, Katavi na Rukwa, walihudhuria kongamano hilo pamoja na...

Thursday, November 22, 2012

SEHEMU YA PILI: Mahojiano ya moja kwa moja na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe katika JamiiForums

MHOJAJI: Mkuu Zitto nashukuru kwa majibu yako kina kwa swali la kwanza, swali linalofuata; B. Zitto na CHADEMA 1) Nini kipaumbele chako cha sasa kama mwanachama wa CHADEMA? 2) Mkuu, ni kweli kuwa CHADEMA ni chama cha kidini/kikabila? Na kama ni kweli, tatizo hilo lishughulikiwe vipi? Kama si kweli, unaweza kuueleza umma wa watanzania una kauli gani juu ya mitizamo hii dhidi ya chama chenu? 3) Mh. Zitto, unaizungumziaje demokrasia ndani ya chama chako katika chaguzi, teuzi na kupanga safu za uongozi? 4) Kwanini CHADEMA haiwatumii viongozi wa Mikoa na Wilaya na badala yake inatuma watu toka makao makuu hata kwa mambo madogo madogo ambayo yangemalizwa na uongozi wa ngazi husika? 5) ...

Wednesday, November 21, 2012

KAMA HUKUPATA NAFASI YA KUSOMA MAHOJIANO YA ZITTO KWENYE JAMII FORUM NAKULETEA MAHOJIANO YA AWALI

>>MASWALI NA MAJIBU YA ZITTO KABWE NA JF  ZITTO:Re: Mahojiano ya moja kwa moja na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe katika JamiiForums Awali ya yote itoe shukrani zangu za dhati kwa kupewa fursa hii adimu ya kuhojiwa na wana JF wenzangu. Nashukuru pia kwa kuwa ni heshima kubwa sana kwangu maana mimi ni mtu wa pili kufanyiwa mahojiano kama haya baada ya kijana mwenzetu Maxence kama 'founder' wa jukwaa letu. Napenda pia ifahamike kuwa mimi ni mmoja wa wanachama waanzilishi wa jukwaa hili na ninafurahi kuona limekuwa na kwa kweli its a force to reckon with. Zitto ni Mtanzania aliyezaliwa Kigoma, Kijiji cha Mwandiga. Nimekulia katika kitongoji cha Mwanga, nimekwenda shule ya Msingi Kigoma, Sekondari Kigoma, Kibohehe Moshi, Galanos Tanga na Tosamaganga Iringa. Nimepata...

MAHOJIANO YA ZITTO KABWE LIVE MUDA HUU JAMII FORUM

Mahojiano ya moja kwa moja yameanza katika thread hii - Mahojiano ya moja kwa moja na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe katika JamiiForums Na hivyo mnakaribishwa kufuatilia, thread hii ni kwa ajili ya side comments na ile ya mahojiano itaendeshwa na AshaDii na atakuwa anajibizana na Mhe. Zitto. FUATILIA MAHOJIANO HAYO HAPA KWA KUBONYEZA LINK HII>>>>>>>>>>>>>>>>>>  ...

Monday, November 19, 2012

J.K ni Jembe. ## MAKALA FUPI KUTOKA KWA MJENGA WA "JF"

Haina ubishi kuwa J. Kikwete ni rais pekee ametawala kwa mizengwe lakini namna anavyoipangua mizengwe hiyo, anastahili pongezi kubwa. Ikumbukwe zengwe la kwanza ni lile la kukataliwa na CHADEMA kuwa si rais halali, wakaenda mbali zaidi kwa wabunge wake kumzilia hotuba yake ya ufunguzi na kutoka nje ili kumdhalilisha, huku katibu mkuu kutangaza kuwa atahakikisha J.K hatawali. Kikwete kwa umahiri mkubwa alitulia na kuendelea kuhutubia huku akiwahakikishia kuwa "ipo siku watarudi kwake" (walirudi hawakurudi?). Zengwe lingine ni la kudai kumshtaki J.K kwa wananchi ili kumshinikiza aondoke madarakani. Hili pia lilifanywa na CHADEMA kupitia maandamano sehemu mbalimbali za nchi wakilenga zaidi kutengeneza propaganda ya kuidanganya jumuiya ya kimataifa kuwa J.K hakubaliki na wananchi. Hilo...

HII IMETOKA JAMII FORUM KAMA ILIVYO### Kauli tatu tata za mwenyekiti wa CHADEMA (Freeman Mbowe) ktk kipindi kisichozidi miezi 3 JE KUNA UKWELI WOWOTE

Kauli tatu tata za mwenyekiti wa CHADEMA (Freeman Mbowe) ktk kipindi kisichozidi miezi 3 WAKUU WANA-JF Kwa kipindi kisicho zidi muda wa miezi mitatu(3) kumekuwa na lugha ama sentesi kadhaa kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa ambazo wachambuzi wa kisiasa kama sisi ni lazima tuzijadili kwa kina kwa sababu hatujawahi kuzisikia kutoka kinywani kwa Kiongozi huyu siku za nyuma pia ni haba sana kuzisikia hasa kwa CHAMA MAKINI KAMA CHADEMA katika taifa hili. Mbowe akiwa kama nguzo imara ya upinzani na amekuwa na machngo mkubwa sana katika harakati za ukombozi ndani ya taifa hili,Lakini lugha zake za hivi karibuni zina ukakasi mkubwa sana pia ni tata kwa wananchi ambao wanaamini kabisa CHADEMA kinaweza kuwa chama mtambuka cha ukombozi ndani ya taifa...

Wednesday, November 14, 2012

KIKWETE MWENYEKITI TENA CCM, MANGULA, DK, SHEIN MAKAMU WAKE

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Makamu wenyeviti wawili, Spika wa Bunge Anna Makinda, baada ya kumtangaza kushinda nafasi hiyo ya Uenyekiti, katika uchaguzi uliofanyika hivi punde katika ukumbi wa Kizota, Dodoma, ikiwa ni kuhitimisha shughuli za Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM. Wapili Kulia ni Makamu Mwenyekiti Mpya wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dk. Moahamed Gharib Bilal Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Jakaya Kikwete na Makamu wake wawili Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (Zanzibar) na Philip Mangula (Bara) wakiwa meza kuu...

HALMASHAURI KUU YA TAIFA YAFANYA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA.

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama Whitehouse mjini Dodoma,leo tarehe 14th Nov 2012. Kikao hicho kitajadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa na Mwenyekiti wa ChaCha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa. Ambapo Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na Mhe. Abdulrahaman...

KUTOKA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFAMakamba azima kura za maruhani

  *Kikwete apeta kwa kushindo   *Kura zapigwa kufuata mikoa Wajumbe mbalimbali katika upigaji wa kura Katika kile kilichoonekana kuepusha jaribio la baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupiga kura ya maruhani dhidi ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete,  Katibu Mkuu Mstaafu, Yusuf Makamba, jana aliuteka Mkutano Mkuu wa Chama hicho kwa kuwapiga vijembe wanachama wanaodaiwa kupanga njama hizo. Makamba alipewa fursa ya kumnadi Rais  Kikwete kwenye mkutano huo muda mfupi kabla wajumbe kupiga kura za mwenyekiti. Kabla ya Makamba kumnadi Rais Kikwete, Naibu...

WANA CCM DIASPORA WATIA FORA KIZOTA, DODOMA

WANA CCM DIASPORA WATIA FORA KIZOTA, DODOMA  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa juu wa CCM katika picha ya pamoja na viongozi wa matawi ya CCM ughaibuni (mkoa wa Diaspora) wakiwa katika mkutano Mkuu wa nane wa chama hicho huko Kizota mjini Dodoma leo  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisalimiana na  viongozi wa matawi ya CCM ughaibuni (mkoa wa Diaspora) wakiwa katika mkutano Mkuu wa nane wa chama hicho huko Kizota mjini Dodoma leo  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Katibu wa CCM tawi la Diaspora UK  Mariamu...

Tuesday, November 6, 2012

Pigo kubwa Chadema Madiwani, Mkurugenzi, Makatibu Wakutwa na hatia

  Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Mwanza imewatia hatiani viongozi watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwamo madiwani wawili kwa kosa la kukaidi amri ya Mahakama. Viongozi waliotiwa hatiani ni madiwani Dan Kahungu wa Kata ya Kirumba na Josephat Manyerere wa Kata ya Nyakato ambaye kabla ya kuondolewa kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye alikuwa ndiye Meya wa Jiji la Mwanza. Viongozi wengine wa Chadema waliotiwa hatiani na Mahakama hiyo ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema Taifa, Benson Kigaila, Katibu wa Chadema Wilaya ya Ilemela, John Anajus na Katibu Mwenezi wa wilaya hiyo, ...

Monday, October 29, 2012

Uchaguzi wa madiwani vurugu tupu

*Mkoani Arusha risasi za moto zarindima mchana kweupe*Songea, wafuasi wa CCM, CHADEMA wakatana mapanga*Chadema yashinda Ludewa, CCM yashinda SongeaMBUNGE wa Viti Maalum, Rahel Mashishanga (CHADEMA) pamoja na Katibu wa Chadema Jimbo la Nyang’hwale mkoani Geita, Michael Ndege, wamenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa na kisha kupigwa na kukatwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Viongozi hao walivamiwa jana katika matukio tofauti, ambapo Mashishanga anadaiwa kuvamiwa jana asubuhi, alipokuwa akiangalia mwenendo wa uchaguzi wa udiwani katika vituo vya kupigia kura, katika Kata ya Mwawaza, mkoani Shinyanga. Akiwa katika kazi hiyo, inasemekana mbunge huyo alivamiwa na kundi la vijana, wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM. Akizungumza na MTANZANIA jana kwa...

Friday, September 28, 2012

CCM YASHINDA UMEYA JIJI LA MWANZA

UFAFANUZI KILICHOTOKEA KWENYE UCHAGUZI WA UMEYA WA JIJI LA MWANZA KATI YA CCM NA CHADEMA. Mgombea wa kiti cha umeya katika Halmashauri ya jiji la Mwanza kupitia CCM na diwani wa kata ya Mkolani Ndg Stanslaus Mabula, ameshinda kiti cha Umeya wa Halmashauri ya Nyamagana kwa jumla ya kura 11 dhidi ya mgombea wa CHADEMA diwani wa kata ya Mahina Ndg Charles Chibara aliyepata kura 8. CCM wameshindishwa na mbinu za kisiasa amabzo uhalali wake kisheria linabaki kuwa suala la wanasheria wanaojua taratibu zikoje kutufafanulia. Baada ya mgawanyo wa Halmashauri ya jiji la Mwanza na kuwa na halmashauri ya jiji inayoundwa na Majimbo mawili, kulipatikana Halmashauri ya Nyamagana inayoundwa na Jimbo la Nyamagana na halmashauri ya ilemela inayondwa na jimbo la Ilemela. Mgawanyo huo ulifanyika...

Thursday, September 27, 2012

ZITTO KABWE KUGOMBEA URAISI 2015

Mbune wa Kigoma  mh. ZITTO KABWE athibitisha kwamba atagombea URAIS 2015,   hayo ameyasema wakati akihojiwa na mwendesha kipindi cha amplifire Millard Ayo. Zitto kupitia amplifer ya CLOUDS FM akasema ya kwamba Atagombea kupitia CHADEMA kwa hivyo wale mlio na wasiwasi huo ndio ukweli. Asema kuna watu wanajidai wao ni CHADEMA zaidi ya wengine wakati yeye amekuwa mwanachama wa CHADEMA tokea ana miaka 16...... Miaka 10 ya ubunge inamtosha hivyo anataka kwenda hatua nyingine kisiasa na anazo AGENDA za msingi za kusimamia hivyo yeye ni tofauti na wanasiasa wengine wanaoutaka urais kama sifa    source; CLOUDS FM ANPLIFER NA MILLAD AYO "}" href="https://www.facebook.com/groups/tanurulafikra/379769648760461/?notif_t=group_activity#" id=".reactRoot[18]" title="Like...

COMRADE SAMABALA AGOMBEA UENYEKITI WA UVCCM MKOA WA DODOMA

       Mwanasiasa na mwanzilishi wa group maarufu la Tanuru la Fikra katika mtandao maarufu wa facebook, hatimaye amefunguka na sera ambazo zitamwingiza kwenye cheo hicho chipya endapo kama wanachama wa Dodoma (UV-CCM) watamchagua katika kinyang'anyiro hicho. na haya ndio maneno yake kwenye ukurasa wa facebook ‎>----SAFARI NDEFU YA MAFANIKIO INAENDELEA--------> *...SHUKRANI ZANGU KWA WOTE NINAOWAPENDA...* Ndugu zangu wana TANURU LA FIKRA Na Watanzania wenzangu wote kwa Ujumla. Jioni ya Leo napenda kuchukua fursa hii kusema Machache kwenu.:- 1. Kwanza Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu...

Pages 51234 »
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Blogger