WAKUU WANA-JF
Kwa kipindi kisicho zidi muda wa miezi mitatu(3) kumekuwa na lugha ama
sentesi kadhaa kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa
CHADEMA taifa ambazo wachambuzi wa kisiasa kama sisi ni lazima
tuzijadili kwa kina kwa sababu hatujawahi kuzisikia kutoka kinywani kwa
Kiongozi huyu siku za nyuma pia ni haba sana kuzisikia hasa kwa CHAMA
MAKINI KAMA CHADEMA katika taifa hili.
Mbowe akiwa kama nguzo imara ya upinzani na amekuwa na machngo mkubwa
sana katika harakati za ukombozi ndani ya taifa hili,Lakini lugha zake
za hivi karibuni zina ukakasi mkubwa sana pia ni tata kwa wananchi ambao
wanaamini kabisa CHADEMA kinaweza kuwa chama mtambuka cha ukombozi
ndani ya taifa hili.
KAULI TATA AMBAZO ZINAZUA MASWALI MENGI KUTOKA KWA MH:FREEMAN AIKAEL MBOWE NI HIZI
1. Kupitia gazeti la majira la wiki tatzu
zilizopita Mh.Freeman mbowe alinukuliwa akisema Yupo tayari kuachana na
chadema wakati wowote atakapo amua.
Kauli hii ni tata na mlengo wake unazua maswali mwengi sana.Tujiulize
mbowe anasema kuwa anatakuacha na siasa za CHADEMA wakati wotete Je ni
kwamba amechoka kupigana na CCM?Au ameshavuna mazao ya siasa na hahitaji
tena kuendelea kuyala?Naweza kwenda mbali kabisa kwamba Mbowe
anapotangaza kuachana na siasa za CHADEMA ni kwamba anataka
kuudhihirishia umma kuwa CHADEMA si mali yake(familia) kama wengi
wanavyokitafsili?
Lakini kauli kama hii mbowe haoni kama anakatisha tamaa kwa viajana
ambao wamekuwa wakijiunga na CHADEMA kutokana na yeye kuwa mwanaharakati
makini kwa muda mrefu?
2. Kupitia GAZETI LA TANZANIA DAIMA wiki iliyopita
Mh.Mbowe alitangaza kumkaribisha waziri mkuu wa zamani Mh.Fredrick
sumaye kwenye ulimwengu wa siasa za CHADEMA.
Swala hili hakika linazua maswali mengi sana.Ikumbukwe SUMAYE ni mmoja
ya mafisadi papa wa nchi hii na alikuwemo kwenye LIST OF SHAME
iliyosomwa na CHADEMA pale mwembe yanga.Je sumaye ameshakuwa msafi kiasi
kwamba anapewa nafasi na CHADEMA?
Kelele za chadema siku zote ni kupingana na rushwa iweje leo mtuhumiwa
mkubwa wa rushwa nchini kama sumaye aonekane muhimu mbele ya chadema na
hatimaye kumtaka asajiliwe?
Lakini tuende mbali zaidi yawezekana MBOWE anamuita SUMAYE aje chadema
kwa ile kauli ya WANYUMBANI NJOO NIKUSHIKE MKONO SIPO RADHI UFIE
JANGWANI hatakama ni haramu??????.........ni siku chache sana SUMAYE
amebwagwa kwenye uongozi ndani ya ccm na ameishia kulalama kuhusu
kufanyiwa mchezo mchafu.
3. Kauli ya tatu tata zaidi ni ile aliyoitoa pale
HAI alipokuwa anamkaribisha na kumshukuru Mh.Rais kikwete kwa utendaji
wake.Mbowe alinukuliwa akisema"nimetembea angani na aridhini Tanzania
nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya
KIKWETE."
Nachelea kusema maneno hayahaya yangesemwa na chama chochote kingine
yangezua gumzo,au yange semwa na mwanachadema yeyote yule yangezua
mjadala mkubwa wakitaifa.
Naomba kuuliza hii ni kauli sahihi ya kiongozi wa upinzani kumwambia
Rais wa nchi hata kama ana show appriciation ya kile
kilichofanyika?Hakuna lugha nyingine yakipinzani-yakusifia
ambayoingetumika hapa???
Mbowe
huu ni wakati wakuwekana wazi kwa watanzania, KAMA UKOMBOZI UMESHAUZWA
NI HERI WATANZANIA WAKAAMBIWA kuliko maneno kama haya ya kusifia
kupitiliza as if nchi hii hakuna upinzani.
WANA-JF nawasilisha naomba tujadiliane kwa makini namna kauli hizi zinavyoathiri chama na zinavyojenga chama.
0 comments:
Post a Comment